Ujumbe wa Kwaresima kuhusu Msamaha


Huruma ya Mungu hutuvuta kila wakati tunapoanguka katika dhambi. Moyo wa mtu uliovunjika na kuguswa hupata maumivu na kuimba Huruma ya Mungu, Mtu huyo mdhamdi aijongeapo altare ya Huruma ya Mungu kwa dhati na unyenyekevu huchota neema tele na kuhuishwa nafsi yake.
Tendo la kuomba Huruma ya Mungu huitwa Toba au Msamaha au Upatanisho au Maungamo au Uongofu au Kitubio. Mgonjwa huhisi uchungu na chuki kubwa dhidi ya dhambi alizozifanya kisha huomba msamaha kuanzia katika nafsi yake, kwa jilani yake na kisha kwa Muumba wakee.Tendo hili takatifu hujitokeza kwa namna mbalimbali kama vile kwa njia ya sala, kufunga, kutoa sadaka, kujinyima, kufanya matendo mema, kuacha uchoyo na ubinafsi na kisha kufanya mageuzi ya rohoni. Namna hizi hazifanyiki tuu katika kipindi cha Kwaresima, bali hupaswa kutekelezwa na Mkristo katika maisha yake ya kila siku.
Roho mtakatifu ni mfanyakazi na mchumba katika roho ya mtu. Huiongoza nafsi na kumsaidia Muungamaji kutafiti dhambi kwa umakini, kufanya majuto kwa masikitiko, kuungama dhambi na kisha kutimiza malipizi.
Wakristo wenzangu, Sakramenti hii ya kitubio hutupatanisha na Mungu, kanisa, kurudishiwa hali ya neema iliyopotea baada ya kutenda dhambi, kuondolewa adhabu ya milele iliyostahiliwa, twapata amani na utulivu wa dhamili, pamoja na faraja ya roho, na mwisho twapata nguvu za Kiroho kwa mapambano ya Kikristo.

This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteEe Yesu tunakutumainia!
ReplyDeleteujunbe mzuri
ReplyDelete