PENDO LISILO NA MWISHO
PENDO LISILO NA MWISHO Ndugu msomaji, Mungu ni upendo ! upendo wake ulijificha ndani ya "Neno" kabla hajauumba ulimwengu. Kwa Hekima yake ya ajabu inayopita ufahamu wa kibinadamu na yanye kuhuishwa na pendo lake, aliumba vyote vilivyomo Mbinguni na Duniani kwa neno la upendo. Katika uumbaji wake Mungu alimuumba mwanadamu kwa sur yake halisi. Hivyo pendo lote la Mungu lilitua katika wazo na Hekima ya kumuumba mwanadamu ili apate kuwa mkamilifu mwenye neema zote za kiroho na kimwilikulingana na kipimo cha Mungu. Licha ya kumuumba mwanadamu, Mungu alimweka mahali pazuri Bustanini ili (w)apate kuvitawala vyote vilivyomo na kufurahia uzuri wake huku akimwabudu, kumtukuza, kumsifu na kumwomba lolote atakalo ilimladi tu lifanane na mapenzi ya muumba wake. Mwanadamu...