PENDO LISILO NA MWISHO

                                          PENDO LISILO NA MWISHO
     Ndugu msomaji, Mungu ni upendo! upendo wake ulijificha ndani ya "Neno" kabla hajauumba ulimwengu. Kwa Hekima yake ya ajabu inayopita ufahamu wa kibinadamu na yanye kuhuishwa na pendo lake, aliumba vyote vilivyomo Mbinguni na Duniani kwa neno la upendo.
     Katika uumbaji wake Mungu alimuumba mwanadamu kwa sur yake halisi. Hivyo pendo lote la Mungu lilitua katika wazo na Hekima ya kumuumba mwanadamu ili apate kuwa mkamilifu mwenye neema zote za kiroho na kimwilikulingana na kipimo cha Mungu.
     Licha ya kumuumba mwanadamu, Mungu alimweka mahali pazuri Bustanini ili (w)apate kuvitawala vyote vilivyomo na kufurahia uzuri wake huku akimwabudu, kumtukuza, kumsifu na kumwomba lolote atakalo ilimladi tu lifanane na mapenzi ya muumba wake.
     Mwanadamu huyo wa kwanza yaani Adamu na Hawa aliishi kwa nguvu na msukumo wa upendo wa Munguhata wanyama wengine walimpenda na kutaka kuishi  karibu ama pamoja naye. Twaweza kusema kuwa maisha yao Adamu na Hawa yalikuwa ni harufu nzuri ya upendo wa Mungu sawa na harufu ya Ua zuri ambalo huweza kufuatwa na Vipepeo wazuri kila wakati. Ama hakika Bustani ya Edeni ilikuwa na harufu ya pendo la Mungu; na zaidi mahali walipoishi Adamu na Hawa.
     Ndugu msomaji wangu, maisha hayo mazuri na ya furahaaliyomilikishwa mwanadamu wa kwanza hayakuendelea hivyo. Hii inatokana kwamba Malaika-mwasi yaani Ibilisialiyetupwa na Mungu Duniani alimshawishi mwanadamu huru kufanya jambo alilokatazwa na Muumba wakeyaani kutokula Tunda la Mti wa ujuzi wa mema na mabaya. HIvyo tangu wakati ule wa kutotii Amri hiyo waliyopewa na Mungu, Mwanadamu alikosa neema ya utakaso ambayo hapo mwanzo iliwafanya wawe na kila fadhila inayotokana na upendo hivyo hata urafiki wao na viumbe wengine ukapungua. Na hasa hii ni kwa sababu ya kutotaka kuomba msamahakwa Mungu ili awarudishie neema hiyo. Hivyo kiburi na tamaa mbaya ya kutaka kufanana na Munguviliwaponza! Itaendelea.........

Comments

  1. Fuatilia makala hii uapate kujua Mungu ni nanai katika maisha yako!

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Ujumbe wa Kwaresima kuhusu Msamaha

THE MEANING OF TRUE HAPPINESS (maana ya Furaha ya Kweli)