[​IMG]Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkinga imekamata shehena ya mafuta ya Taa kutoka nchi jirani ya Kenya yaliyoingizwa nchini bila kulipiwa ushuru kwa madai kuwa baadhi ya wafanyabiashara hulazimika kupitisha bidhaa hiyo kwa njia za panya kisha kuingizwa nchini kinyume cha sheria madai kuwa mafuta hayo huuzwa kwa bei rahisi nchini Kenya baada ya Serikali ya Tanzania kupandisha bei 

Wakizungumza wakati kamati hiyo hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkinga Mark Yona kufanya operesheni katika kijiji cha Jesini kilichopo jirani na Kenya. Afisa Uhamiaji wa wilaya pamoja na mkuu wa kikosi maalumu cha kuzuia magendo katika eneo la Moa lililopo mpakani mwa nchi hizo mbili, wamesema mafuta ya Taa yamekuwa yakiingizwa kwa wingi hasa baada ya Serikali ya Tanzania kupandisha bei ya bidhaa hiyo. 

Katika zoezi hilo la kuhakikisha sheria za nchi zinaimarishwa, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkinga Mark Yona amesema katika kipindi cha miezi mitatu wamekamata magunia ya mkaa 325 huku miti aina ya mikoko 1500 iliyokuwa ikisafirishwa nchini Kenya baada ya baadhi ya wafanyabiashara kumaliza miti hiyo katika fukwe za bahari ya hindi nchini Kenya na kuanza kuingilia ya hapa nchini. 

Kufuatia hatua hiyo meneja wa Wakala wa misitu wilayani Mkinga Frank Chambo ameshukuru kwa operesheni inayoendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama wilayani Mkinga katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na baadhi ya raia wa Kenya kwa kuvuna mikarambati na mikoko na kusafirishwa nchi jirani ya Kenya kwa sababu wao wanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa usafiri wa majini ili kudhibiti tatizo hilo.

Comments

Popular posts from this blog

Ujumbe wa Kwaresima kuhusu Msamaha

THE MEANING OF TRUE HAPPINESS (maana ya Furaha ya Kweli)