Posts

Showing posts from February, 2015

Maisha ya Fadhila na changamoto za wakristo wa mashariki ya mbali.

Hivi karibuni tumeshuhudia mauaji ya wakristo 21 nchini Libya. Hicho ni kielelezo kidogo tosha juu ya mateso wanayoyapata wakristo hasa wanaoishi katika nchi za kiislamu. Mafundisho ya Kristo bwana na mwokozi wetu yanatuonya tusilipize kisasi bali tuwe wavumilivu na wenye subira tukiwaombea maadui zetu na kuwapenda upeo! Fadhila kuu ya mapendo hujengwa ndani ya nafsi ya binadamu mahali na katika mazingira ya utulivu na kupima kila jambo kwa hekima ya kimungu.....

PENDO LISILO NA MWISHO

                                          PENDO LISILO NA MWISHO      Ndugu msomaji, Mungu ni upendo ! upendo wake ulijificha ndani ya "Neno" kabla hajauumba ulimwengu. Kwa Hekima yake ya ajabu inayopita ufahamu wa kibinadamu na yanye kuhuishwa na pendo lake, aliumba vyote vilivyomo Mbinguni na Duniani kwa neno la upendo.      Katika uumbaji wake Mungu alimuumba mwanadamu kwa sur yake halisi. Hivyo pendo lote la Mungu lilitua katika wazo na Hekima ya kumuumba mwanadamu ili apate kuwa mkamilifu mwenye neema zote za kiroho na kimwilikulingana na kipimo cha Mungu.      Licha ya kumuumba mwanadamu, Mungu alimweka mahali pazuri Bustanini ili (w)apate kuvitawala vyote vilivyomo na kufurahia uzuri wake huku akimwabudu, kumtukuza, kumsifu na kumwomba lolote atakalo ilimladi tu lifanane na mapenzi ya muumba wake.      Mwanadamu...