Habari
NAISHUKURU MAHAKAMA IMETENDA HAKI
Mama wa marehemu Stephen Kanumba akizungumza baada ya Mahakama Kuu kumhukumu @elizabethmichaelofficial kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kumuua bila kukusudia Stephen Kanumba https://www.facebook.com/MwananchiNews/videos/10155909395889339/
Bodi ya Mikopo yatangaza orodha mpya ya mikopo>http://bit.ly/2zAVbH4
RC Luhumbi atoa siku 40 mradi wa maji ukamilike>http://bit.ly/2yv4m8A
UKWEPAJI KODI: Mamlaka ya Mapato nchini Rwanda imesema itapiga mnada mali za familia ya Rwigara ili kufidia deni la kodi takribani Dola Milioni 6.
- Ili kunusuru mali zao, wametakiwa kulipa deni hilo ndani ya mwezi huu (Novemba, 2017)
Zaidi, soma => https://goo.gl/GhWyya
Watu wanne wamekamatwa nchini Zimbabwe wakituhumiwa kumzomea mke wa rais wa nchi hiyo Grace Mugabe wakati akihutubia mkutano wa hadhara siku ya jumamosi iliyopita.
Gazeti linalomilikiwa na Serikali la The Herald limeripoti kwamba watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kupuuza mamlaka ya rais.
Kuzomea huko kuliibuka kati ya makundi mawili ndani ya chama tawala cha Zanu-PF yanayopambana juu na nani atakuwa mrithi wa rais Robert Mugabe ambapo kuna kundi linalimuunga mkono mke wa rais Grace Mugabe na lile linalomuunga mkono Makamu wa rais aliyefukuzwa Emmerson Mnangagwa.
Imedaiwa kwamba watu hao waliokamatwa ni wafuasi wa aliyekuwa Makamu wa Rais
Watu hao walikamatwa mara baada ya mkutano huo uliofanyika mjini Bulawayo,watuhumiwa hao inasemekana ni aliyefukuzwa Emmerson Mnangagwa .
Watuhumiwa hao waliokatwa ni wanaume watatu na mwanamke mmoja wako nje kwa dhamana.
Chanzo: EATV
DIWANI wa Kata ya Mabuki, Nicodemas Ihano (CCM) na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwanangwa kilichopo wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza, Faustine Malago (CCM), wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuvunja nyumba, kuiba na kuchoma moto mali za mwekezaji.
Ihano ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na wenzake watatu, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya hiyo na kusomewa hati za mashtaka matatu ambapo walikana mashtaka yanayowakabili na wote wako nje kwa dhamana.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Russy Mkisi, Mwendesha Mashtaka wa polisi, Ramsoney Salehe, aliiambia Mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja Oktoba 24, mwaka huu saa 7.00 mchana kwenye Kijiji cha Mwanangwa eneo la machimbo ya madini ya almasi, walikula njama na kuvunja nyumba na kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh milioni 2.8.
Salehe alisema tuhuma nyingine zinazowakabili washtakiwa hao ni kuchoma moto nyumba na magari mawili vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 170.8 mali ya Badar Sudi mkazi wa Shinyanga ambaye ni mwekezaji na mchimbaji wa kati wa madini ya almasi katika Kijiji cha Mwanangwa.
Watuhumiwa wote walikana mashtaka yanayowakabili ambapo walikidhi masharti ya dhamana iliyowataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wenye mali isiyohamishika na wote wako nje kwa dhamana ya Sh milioni 5 kila mmoja.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Stephano Bengwe (32) na Herddius Gwido (40), wote wakazi wa Kijiji cha Mabuki, ambapo Hakimu Mkazi Mfawidhi, Russy Mkisi, aliahirisha kesi hiyo ambapo itatajwa tena Novemba 14, mwaka huu.
Chanzo: Mtanzania
SINGIDA: Watu wawili wamefariki dunia baada ya gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili za T862 DJW kugongana na basi la Taqwa lililokuwa linatokea Kampala eneo la Kidaka lililopo Wilaya ya Ikungi
Wakizungumza wakati kamati hiyo hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkinga Mark Yona kufanya operesheni katika kijiji cha Jesini kilichopo jirani na Kenya. Afisa Uhamiaji wa wilaya pamoja na mkuu wa kikosi maalumu cha kuzuia magendo katika eneo la Moa lililopo mpakani mwa nchi hizo mbili, wamesema mafuta ya Taa yamekuwa yakiingizwa kwa wingi hasa baada ya Serikali ya Tanzania kupandisha bei ya bidhaa hiyo.
Katika zoezi hilo la kuhakikisha sheria za nchi zinaimarishwa, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkinga Mark Yona amesema katika kipindi cha miezi mitatu wamekamata magunia ya mkaa 325 huku miti aina ya mikoko 1500 iliyokuwa ikisafirishwa nchini Kenya baada ya baadhi ya wafanyabiashara kumaliza miti hiyo katika fukwe za bahari ya hindi nchini Kenya na kuanza kuingilia ya hapa nchini.
Kufuatia hatua hiyo meneja wa Wakala wa misitu wilayani Mkinga Frank Chambo ameshukuru kwa operesheni inayoendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama wilayani Mkinga katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na baadhi ya raia wa Kenya kwa kuvuna mikarambati na mikoko na kusafirishwa nchi jirani ya Kenya kwa sababu wao wanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa usafiri wa majini ili kudhibiti tatizo hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akishikana mkono na kupongezana na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi litakalo toka Hoima nchini Uganda hadi eneo la Chongoleani mkoani Tanga.
Sherehe za uwekaji wa jiwe hilo zimefanyika katika eneo la Mutukula Wilayani Kyotera nchini Uganda
Barua ya Katibu Mkuu CCM kuhusu kujiuzulu kwa Nyalandu “tulishaanza kumchukulia hatua”
Moja ya habari kubwa za sasa hivi nchini Tanzania ni Lazaro Nyalandu ambae juzi ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Ubunge wa Singida Kaskazini.
Baadae Spika Ndugai alihojiwa na vyombo vya habari na kusema kwamba pamoja na kusikia taarifa za kujiuzulu kwa Nyalandu kwenye vyombo vya habari, yeye bado hajapokea barua ya kujiuzulu kwa Mbunge huyo.
Sasa leo imetoka taarifa kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma ikiwa imeandikwa kama inavyosomeka hapa chini…
Ofisi ya Spika ingependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM) Ndugu Lazaro Nyalandu ambayo amekuwa akiarifu kwamba amemwandikia Mheshimiwa Spika kumtaarifu kujiuzulu kwake.
Hata hivyo, Mhedhimiwa Spika amepokea barua toka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ya tarehe 30 Oktoba, 2017 akimuarifu kwamba kwa muda sasa Chama hicho kilishaanza kumchukulia hatua za kiudhibiti na kinidhamu dhidi ya vitendo na kauli zake zisizoridhisha kinyume na misingi, falsafa na itikadi ya Chama cha Mapinduzi.
Hivyo, Chama cha Mapinduzi kuanzia tarehe ya barua yao kimemjulisha Mheeshimiwa Spika kuwa Ndugu Lazaro Nyalandu amepoteza sifa za Uanachama wa Chama cha Mapinduzi, na hivyo kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa Chama hicho na Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya Chama hicho.
Mheshimiwa Spika, angependa kuwaarifu Watanzania kwamba kwa barua hiyo toka mamlaka halali ndani ya Chama cha Mapinduzi ambacho Ndugu Lazaro Nyalandu alipata Ubunge kupitia Chama hicho na kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotamka kwamba:
“Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake cha Ubunge iwapo litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo: (f) Iwapo Mbunge ataacha kuwa Mwanachama cha chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.”
Hivyo, Ndugu Lazaro Nyalandu si Mbunge tena na hatua stahiki za kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa.
Comments
Post a Comment