Watu Maarufu
Leo tar. 09.12.2017, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemsamehe mwanamziki Babu Seya aliyekuwa amefungwa katika gereza la Ukonga jijini
Dar es Salam.
.
Maisha ya Safiya, Mtanzania anayefanya kazi China>http://bit.ly/2miVtgnTukiwa #Morogoro , @vanessamdee alieleza kwamba @juma_jux amekuwa akiomba sana warudiane lakini yeye bado hajakubali.
Alisema nafasi ya mwisho kwa Jux itakuwa #TigoFiestaKubwaLao hapa Dar es Salaam ambapo Jux atapewa dakika 15 za kumshawishi V warudiane.
#TigoFiesta2017 DSM ni November 25, Je @juma_jux na @vanessamdee wataruadiana jukwaani?
Alikuwa muimba #Kareoke tu, mwaka 2016 ndipo alipata nafasi ya kujaribiwa kwenye ligi kuu ya burudani.
#TigoFiesta2017 imezidi kudhihirisha ubora wake kwani mwaka huu anatajwa kuwa kati ya ya wasichana wachache wanaofanya vizuri kwenye muziki.
Leo katajwa kwenye orodha ya kwanza ya wasanii wataopiga #TigoFiestaKubwaLao lakini pia leo ni siku yake ya kuzaliwa.
#HappyBirthdayNandy, Wasalimie Nigeria: Dar inakusubiri. @officialnandy
Tambo na majigambo, #Natamba , @aslayisihaka anatamba.
Kuna maneno kwamba ukitaja wasanii watatu wanaokubalika zaidi Bongo kwa sasa lazima umtaje #Aslay (sio maneno yetu)
Je wewe unakubaliana na hilo?
Tarehe 25 mwezi huu pale Leaders Aslay atakuwa na kibarua kizito kudhihirisha kwamba yeye ni kinara na anastahili kutamba.
.
.
Itakuwa #TigoFiesta2017 na hii ni #TigoFiestaKubwaLao.
.
.
Itakuwa #TigoFiesta2017 na hii ni #TigoFiestaKubwaLao.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Modo Hamisa Mobeto dhidi ya mwanamuziki Diamond Platnumz juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul.
Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Novemba 10 ,2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.
Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.
Mobeto anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.
Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake
Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Sh 5 milioni kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.
Comments
Post a Comment