Siasa

ANNA MGHWIRA AHAMIA CCM RASMI












Balozi wa China awaasa Waandishi wa habari wa Tanzania

  


Serikali ya China imewataka Waandishi wa Habari za Tanzania na China kutumia vyanzo vya uhakika kuhabarisha dunia juu ya uhusiano wenye manufaa baina ya pande mbili hizo badala ya kutegemea vyanzo vya nchi za Magharibi, ambavyo falsafa yake imekuwa ni kuripoti habari mbaya dhidi Taifa hilo na nchi za dunia ya tatu Tanzania ikiwemo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza na wanahabari jijini Dar es salaam , Balozi mpya wa China nchini,WANG Ke, ameviahidi vyombo vya habari kuwa milango iko wazi pale wanapokuwa na shaka juu ya ripoti zinazotolewa kuhusiana na China na kuwaomba wawasiliane na idara yake ya habari na ile ya Diplomasia ya Umma.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Dokta HASSAN ABBAS,amemweleza Balozi huyo vipaumbele na changamoto za vyombo vya habari nchini,hususan teknolojia aliyosema imeviacha nyuma vyombo vya habari nchinasa vile vya asili.

Katika hatua nyingine,Msemaji Mkuu wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, MINDI KASIGA, ambaye hivi karibuni aliongoza timu ya Waandishi wa habari katika ziara ya mafunzo nchini China,ameviomba vyombo vya habari kuwahabarisha fursa zilizoko nchini humo,ambapo amezungumzia manufaa ya mkataba wa kuuza zao la muhogo uliosainiwa baina ya nchi hizo mbili.

Dr Slaa Aajiriwa Kwenye Duka la SuperMarket Canada

 

Aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, ameajiriwa katika duka kubwa la bidhaa za majumbani (Supermarket) la Costco lililopo Oakville, Toronto nchini Canada, imebainika.

Dk. Slaa, kwa sasa anaishi nchini Canada alikokwenda kwa masomo, tangu alipotangaza kuachana na siasa Septemba 1, mwaka 2015.

Kwa muda wa wiki kadhaa, ziliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mbunge huyo wa zamani wa Karatu, amemaliza masomo yake na sasa anafanya kazi katika moja ya maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali nchini humo – Supermarket.

Supermarket ya Costco anayofanya kazi Dk. Slaa akihudumu kama Mshauri wa Mauzo (Sales Advisor), akilipwa Dola za Marekani 10 (zaidi ya Sh 20,000) kwa saa, ina hadhi kama Nakumat, Shopers, Imalaseko, Game na maduka mengine makubwa nchini.

Akizungumza na Gazeti la Mtanzania jana kwa simu , Dk. Slaa alisema kuwa kwa sasa anaishi kwa kazi ya mikono yake  kwani ili aweze kuishi anahitaji kufanya kazi zaidi ya mbili hadi nne kwa siku.

“Niko, ninafuatilia matukio Mutukula (ziara ya Rais Dk. John Magufuli jana). Siku zote nimesema ninaishi kwa jasho na kazi ya mikono yangu. Canada ili uishi vizuri, unahitaji kazi zaidi ya mbili au tatu mpaka nne. Hayo nimeweka wazi, sijui jambo jipya kama mtu alikuwa hafuatilii.

“Mimi ninafanya kazi PWD/CDS/COSTCO kama Sales Advisor, baada ya kumaliza masomo yangu hasa Interpersonal Communication. Costco ninakofanya kazi ina members (wanachama) 10,000.  Kwa siku wanaofika Warehouse ni kati ya 5,000 hadi 7,000,” alisema Dk. Slaa.

Mbali na hilo, alisema kuwa pia anafanya kazi nyingine ikiwa ni pamoja na ushauri (Consultancy).

Alisema kila mara amekuwa akiwataka Watanzania na vijana wafanye kazi kwani fedha haziji kwa kukesha kwenye mtandao wala propaganda.

“Canada ni kazi, Profesa wa Chuo Kikuu anafanya kazi ya Uber. Sijui kama Uber inafahamika Tanzania, ni dereva Taxi kwa kutumia gari lake binafsi. Ofisa wa Serikali usiku anaosha vyombo hotelini.

“Ndiyo maana familia ina magari mawili au zaidi, TV, nyumba ya kisasa, chakula cha kisasa. Wanatekeleza sera ya ‘Hapa Kazi Tu’ kwa matendo. Nadhani nimekupa taarifa za kutosha ikiwa ni pamoja na kujibu propaganda kuwa nilihongwa mabilioni.

“Niwahakikishie tena, wakati wa kusoma nilikuwa na scholarship, tangu nianze kazi ninaishi kwa jasho la mikono yangu. Mke wangu yeye ameingia Chuo Kikuu cha York baada ya Diploma yake na bado anapata scholarship.

“Ndiyo maana tuna uwezo wa kuwa na magari mawili aina ya Jeep na Dodge, ukifanya kazi utaishi vizuri. Hii ni pamoja na kugharamiwa bima ya afya (Health Insurance), watoto kusomeshwa na Serikali ya Canada,” alisema Dk. Slaa.

Mei mwaka huu, Dk. Slaa, alisema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa na kwamba taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli wowote.

Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye alipata kuwa Mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza kuainisha mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na kwenda kuishi ughaibuni.

Septemba, 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Dk. Slaa alijiweka kando na siasa, kwa kile alichokieleza kutofautiana na viongozi wenzake ndani ya chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

“Sina tabia ya kuyumbishwaa, sina chuki na mtu yeyote, sipendi siasa za udanganyifu na propaganda. Nimeachana na siasa tangu Julai 28, 2015, baada ya kuona misingi ya chama nilichoshiriki kukijenga imepotoshwa,” alisema Dk. Slaa siku alipotangaza kuachana na siasa.

Alisema sharti la kwanza ambalo alitaka Chadema izingatie, ni kiongozi huyo wa zamani ndani ya Serikali ya CCM, kujisafisha dhidi ya tuhuma ya kashfa ya sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.

Majaliwa awataka mawaziri wasitoe matamko yasiyotekelezeka










Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

BREAKING: Barua ya Katibu Mkuu CCM kuhusu kujiuzulu kwa Nyalandu “tulishaanza kumchukulia hatua”


Moja ya habari kubwa za sasa hivi nchini Tanzania ni Lazaro Nyalandu ambae juzi ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Ubunge wa Singida Kaskazini.
Baadae Spika Ndugai alihojiwa na vyombo vya habari na kusema kwamba pamoja na kusikia taarifa za kujiuzulu kwa Nyalandu kwenye vyombo vya habari, yeye bado hajapokea barua ya kujiuzulu kwa Mbunge huyo.
Sasa leo imetoka taarifa kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma ikiwa imeandikwa kama inavyosomeka hapa chini…
 Ofisi ya Spika ingependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM) Ndugu Lazaro Nyalandu ambayo amekuwa akiarifu kwamba amemwandikia Mheshimiwa Spika kumtaarifu kujiuzulu kwake.
Hata hivyo, Mhedhimiwa Spika amepokea barua toka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ya tarehe 30 Oktoba, 2017 akimuarifu kwamba kwa muda sasa Chama hicho kilishaanza kumchukulia hatua za kiudhibiti na kinidhamu dhidi ya vitendo na kauli zake zisizoridhisha kinyume na misingi, falsafa na itikadi ya Chama cha Mapinduzi.
Hivyo, Chama cha Mapinduzi kuanzia tarehe ya barua yao kimemjulisha Mheeshimiwa Spika kuwa Ndugu Lazaro Nyalandu amepoteza sifa za Uanachama wa Chama cha Mapinduzi, na hivyo kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa Chama hicho na Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya Chama hicho.
Mheshimiwa Spika, angependa kuwaarifu Watanzania kwamba kwa barua hiyo toka mamlaka halali ndani ya Chama cha Mapinduzi ambacho Ndugu Lazaro Nyalandu alipata Ubunge kupitia Chama hicho na kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotamka kwamba:
“Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake cha Ubunge iwapo litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo: (f) Iwapo Mbunge ataacha kuwa Mwanachama cha chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.”
Hivyo, Ndugu Lazaro Nyalandu si Mbunge tena na hatua stahiki za kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Ujumbe wa Kwaresima kuhusu Msamaha

THE MEANING OF TRUE HAPPINESS (maana ya Furaha ya Kweli)